Sunday, January 27, 2013

KATIBA MPYA TANZANIA

KUMEKUA NA MIJADALA MINGI KUHUSU KATIBA  TUITAKAYO,MUUNDO NA MAMBO MENGI
TUME IMEJITAIDI KUFIKIA WATU KADRI YA MUDA WALIOPEWA KUKAMILISHA HIYO KAZI ILA MAONI MENGI YAMESHIONDWA KUFIKIWA KUTOKANA NA MUDA MCHACHE,JAPOKUA TUME IMETOA BARUA PEPE ILI WALE AMBAO HAWAJATOA MAONO WATOE KUPITIA HUKO,INGAWA TUNAJUA WATANZANIA WACHACHE WANATUMIA TEKNOLOJIA HII NGENI UKILINGANISHA NA IDADI YA WANANCHI
JE WADAU MNAONAJE KUHUSU HILI?
MUDA UONGEZWE?
AU MIJADALA YA REDIO NA LUNINGA ITUMIKE AU NJIA GANI ITUMIKE?

umuhim wa ict katika uhifadhi mazingira na utalii endelevu

kwa karibu miongo 2 tumeshuudia mabadiliko makubwa ya teknolojia  ya mawasiliano(ICT) na kumekua na mijadala mbalimbali kuhusu matumizi ya  teknolojia hii
pamoja na kurahisha kazi pia imekua na  faida hasi kwa jamii km vile kupunguza ajila mfano kazi za watu wawili zaweza fanya na mmoja.
ingawa imeongeza ajira kwa wataalam wa ict inchi kwa kua bado tu wachanga katika hili.
Je mdau wewe unaichukuliaje teknolojia hii hasa katika uhifadhi mazingira asilia na utalii endelevu(nature conservation and ecotourism)

Thursday, January 20, 2011

matamko ya viongozi wa kidini juu ya vurugu arusha


hivi karibu ni tumeshuudia  viongozi bali mbali wa kidini wakitoa matamko mbali mbali,matamko hayo  yapo katika makundi mawili makubwa,maaskofu na mashehe,wapo waliolaaniwazi wazi na wapo waliokwepa kulaani wazi wazi.kuna wengine wamefikia hatuaa ya kuhoji  uhalali wa viongozi hao kutoa tamko
muhimu kujadili
je nafasi ya viongozi wa dini ni ipi katika kuimalisha ustawi wa nchi  inchi?
je viongozi wa dini wana haki ya kutoa tamko?
je demokrasia yetu inakua au inakufa?

KATIBA MPYA TANZANIA

 TANZANIA NI MUUNGANO WA NCHI MBILI YAANI TANGANYIKA NA ZANZIBAR,MUUNGANO HUO UKAZAA SERIKALI MBILI,YA MAPINDUZI NA YA MUUNGANO
    ZANZIBAR WANA KATIBA YAO YA MWAKA 1984 NA TANZANIA IPO YA MWAKA 1977,ZOTE ZIMEFANYIWA MAREKEBISHO MENGI,KUNABAADHI YA WANANCHI  WANATAKA KATIBA MPYA NA WENGINE YA ZAMANI IFANYIWE MAREKEBISHO .
     YOTE YANAWEZEKANA ILA KATIKA KUFANYA HAYO KUNA TATIZO KATIKA HILO  KWANI KUNA AMBAO HAWAPO KATIKA MAKUNDI YOTE MAWILI KUNDI LA MAREKEBISHO NA KUNDI LA KATIBA MPYA,.HAWA NI WENGI KULIKO HAYO MAKUNDI MAWILI  NILIYOTAJA,NI WALE TUSIOJUA KATIBA YETU TULIYONAYO SASA.


MUHIM
TUPO KWENYE MJADALA,TUNATAKA KATIBA YETU IWEJE?
JE MUUNDO WAKE UWE VIPI?
JE TUNAJUA MAPUNGUFU YA KATIBA YA SASA?
MNAOFAHAM TUCHANGIE ILI WENGINE TUJIFUNZE KUPITIA KWENU

Monday, January 10, 2011

MAKABLASHA MENGI MAFANIKIO MACHACHE

Tanzania nio moja ya nchi ambazo  zina mipango mingi ya maendeleo kuanzia na MKUKUTA,MKURABITA,VISION2025  ambayo yote ina mgusa  mwananchi katika  kufanikiwa!

tatizo ni kwamba mambo mengi yapo kwenye maandishi tena kwa lugha ngumu ambapo tunajua sisi watanzania ni wavivu wa kusoma,la pili mlengwa mwenyewe  ajitambui km  mlengwa,tatu ambalo ni kubwa katika lote ni ufungufu wa takwimu  za karibuni(recent data) kwa kuwa hatufanyi tafiti hasa za kmatatizo yanayotusibu eidha kwa kupenda au kwa mfumo tuliojiwekea.HUKU TUKITEGEMEA FEDHA ZA WAFADHILI KTK MAENDELEO NA FEDHA ZETU ZA NDANI(MAPATO YA NCHI)YAKIWA KWENYE BAJETI YA MATUMIZI.
MUHIMU
ANGALIA NAFASI YAKO KM MDAU UTAIFANYIA NINI NCHI
CHANGIA MJADALA TUONE JINSI GANI TUTAINUA MAENDELEO YETU

NAFASI YA UFUGAJI NYUKI KATIKA KUMKWAMUA MTANZANIA

UTANGULIZI
ufugaji nyuki tanzania ni moja ya shughuli zenye historia ndefu hasa ukizingatia tangu karne kadhaa,wazee wetu wameendelea kutumia ASALI na NTA km  vyanzo vya mapato na chakula kwa jamii mbali mbali
.japokua tanzania tuna utajiri wa malisho ya nyuki(bee fodder) lakini  bado kiwango, ubora wa asali unasikitisha!Jamii bado inategemea mizinga ya asili(traditional hive) kuliko aina nyingine za mizinga,mwamko wa wananchi katika ufugaji wa kisasa bado uko chini.idadi ya wataalamu wa fani ya ufugaji nyuki bado haitoshelezi,pia patop la taifa kutokana na kuuza nchi za nje mazao ya nyuki linapungua mwaka hadi mwaka,


JE SERIKALI,NA WATAALAM  HUSIKA WANATIMIZA WAJIBU WAO
?MWANANCHI JE?
NAFASI YA  WADAU WENGUINE KATIKA SUALA HILI NI IPI?
MUHIMU
CHANGIA MJADALA HUU KUPATA SULULISHO